Waigizaji maarufu Marekani Tom Holland na Zendaya wameripotiwa kuchumbiana wakati wa msimu wa Sikukuu uliyopita kwenye moja ya makazi ya familia ya Zendaya.
TMZ imeeleza kuwa uchumba huo ulidhihirika baada ya Zendaya kuonekana akiwa amevalia pete ya uchumba wakati alipohudhuria katika usiku wa tuzo za Golden Globes zilizotolewa Januari 5,2025.
Wanandoa hao, waliokutana walipokuwa wakiigiza kama Peter Parker na MJ katika filamu za Spider-Man, wamekuwa wakihusishwa kimapenzi tangu mwaka 2021 huku mara kwa mara akieleza nia yao ya kuishi pamoja kama mke na mume.
Mbali na hilo la wawili hao kuchumbiana lakini pia Holland kupitia kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni aliweka wazi kuwa atakapojaaliwa kupata watoto basi atastaafu kuigiza na kujikita zaidi katika malezi ya watoto wake pamoja na kucheza gofu.
Katika mahojiano yake na Men’s Health, nyota huyo alielezea hamu yake ya kujiondoa katika uigizaji ni kutaka kushiriki kikamilifu na kuwa baba anayehusika katika malezi ya watoto kwenye kila hatua.
Holland kwa sasa anatarajia kuoneakana katika filamu ya ‘The Odyssey’ iliyoongizwa na Christopher Nolan inayotarajiwa kutoka Julai 17, 2026 akishirikiana na mpenzi wake Zendaya na nyota wengine kutoka nchini humo.
Leave a Reply