Baada ya msanii wa maigizo Rose Ndauka kuachia Ep yake ya Majibu Rahisi mwezi Disemba, 2024 nakupokea maoni mengi ya kumkatisha tamaa, Msanii na Mtangazaji Frida Amani amekuja na maoni yake ambayo yamekuwa tofauti na wengi kwa kuonesha kuukubali muziki Ndauka.
Kupitia ukurasa wake wa X Frida Amani aliandika maneno kuonesha kuukubali muziki wake huku akisema ukiamua kumsikiliza Rose Ndauka kwa vibe la kupenda na sio mjuaji utapenda ngoma zake.
"Ukiamua kumsikiliza Rose Ndauka kwa vibe la mpenda muziki na sio mjuaji wa muzikiutapenda ngoma zake minimependa" ameandika Frida Amani.
Rozzie aliachia Ep ya Majibu Rahisi Disemba 26, 2024 ikiwa na jumla ya ngoma 6 ambazo ni Majibu Rahisi FT Appy, Staki ft Gazza, Achauongo, yuko Wapi Ft Abdul Kiba, Tuko Sawa, Walete.
Maoni yako ni yapi juu ya muziki wa Rose Ndauka?
Leave a Reply