Mwanamuziki Drake bado anaikomalia kampuni ya Universal Music Group (UMG) ambapo ametoa malalamiko mapya akidai kuwa kampuni hiyo ilitumia onesho la Super Bowl lililofanywa na Kendrick Lamar kama silaha ya kumchafua hadharani.
Katika hati mpya ambayo imewasilishwa mahakamani wiki hii Drake ameweka malalamiko akidai kuwa onesho la Super Bowl lilimvunjia heshima ambapo kwasasa malalamiko hayo yanamlenga moja kwa moja Kendrick.
Wakati wa tamasha hili Lamar alidaiwa kutoimba maneno kama “pedophile” katika wimbo Not Like Us kwenye onesho hilo ambapo Drake anadai kuwa hatua ya kuondoa neno hilo hakukuwa kwa kupenda bali imepangwa kwa makusudi.
“Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, Kendrick Lamar hangepewa ruhusa ya kutumbuiza katika Super Bowl isipokuwa neno ‘pedophile’ (katika mstari wa ‘certified pedophiles’) lingeondolewa kwenye mistari ya wimbo hii ni kwa sababu karibu kila mtu anaelewa kuwa ni matusi makubwa na ya kashfa kumuita mtu ‘pedophile’,”imeeleza taarifa hiyo
Ikumbukwe Januari 2025, Drake alifungua kesi ya kashfa dhidi ya kampuni ya Universal Music Group (UMG) katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani, ambapo katika kesi hiyo, alidai kuwa UMG ilichapisha na kukuza wimbo wa Kendrick Lamar uitwao Not Like Us, ambao una madai ya kumchafua kwa kumhusisha na tuhuma za unyanyasaji wa watoto.

Leave a Reply