Hakuna Kipengele Kwenye Kesi Ya Diddy

Hakuna Kipengele Kwenye Kesi Ya Diddy

Imeripotiwa kuwa Jaji wa shirikisho Arun Subramanian ameeleza kuwa kesi ya rapa Sean “Diddy” Combs bado itaendelea kama ilivyopangwa kuanza kusikilizwa mwezi Mei, licha ya timu ya mawakili wa Combs kuomba isogezwe mbele.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mahakamani, Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani, Subramanian, alikataa ombi la kesi hiyo kusogezwa mbele kwa miezi miwili ili Diddy na mawakili wake kupata muda wa ziada kukusanya ushahidi.

Ombi hilo ambalo limewasilishwa mapema wiki iliyoisha na wakili wa Diddy, Marc Agnifilo akiomba kesi hiyo iweze kusogezwa kwa miezi miwili kwani bado hawajajiandaa vizuri kukabiliana na kesi hiyo mwezi Mei.

Hata hivyo, Jaji Subramanian hakukubaliana na ombi hilo. Alifunguka kuwa Diddy tayari ana timu nzima ya mawakili wasiopungua wanne wanaoshughulikia kesi hiyo, hivyo hatakubali kuwapa muda ili kutafuta ushahidi wa bahati nasibu.

Mbali na hilo lakini pia alikataa maombi mengine kadhaa yakiwemo ya kufuta shtaka la tatu na tano, ambayo yote yanahusiana na tuhuma za kusafirisha watu kwa ajili ya biashara ya ngono.

Utakumbuka Combs alikamatwa Septemba 16,2024 jijini New York na maafisa wa Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (Homeland Security Investigations). Huku kesi yake ikipangwa kuanza kusikilizwa Mei 5,2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags