Mwili wa aliyekuwa mwigizaji Carina wapokelewa jijini Dar es Salaam

Mwili wa aliyekuwa mwigizaji Carina wapokelewa jijini Dar es Salaam

Mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu nchini, Hawa Hussein 'Carina' tayari umewasili Uwanja Wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) leo Aprili 18, 2025 kutoka nchini India .

Mwili huo baada ya kuwasili umesomewa dua kisha kupelekwa nyumbani kwao Magomeni Mapipa.

Mwili wa Carina utaswaliwa Masjid Maamur na kupumzishwa katika makabuli ya kisutu kesho Aprili 19, 2025.

Carina alifariki dunia Jumanne Aprili 15, 2025 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya tumbo baada ya kuondoka nchini Februari 24, 2025.

Ikumbukwe Carina aliugua kwa takriban miaka tisa na kupelekea afanyiwe upasuaji zaidi ya mara 26






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags