Priscilla Ojo mfanyabiashara na mwigizaji ambaye ni mke halali wa mwanamuziki Juma Jux amefunguka sehemu ambayo amekutana na mume wake huyo akieleza kuwa walikutana Rwanda.
“Basi tulikutana nchini Rwanda kwenye safari ya kibiashara, halafu nikaonana, naye akaniona kwenye darasa la biashara. Kisha tukakutana tena hotelini, akanipatia namba yake na kunichukua namba yangu pia. Aliniambia nimtumia ujumbe, lakini sikumtumia. Hata hivyo, alivyojua njia yake ya kunifikia, tukaanza kuzungumza na ndiyo, tuko hapa leo.
Nahisi kwamba siku ya kwanza kabisa nilipokutana naye wow ulikuwa usiku wa kipekee sana. Kulikuwa na kitu tofauti kuhusu usiku huo ambacho kilinikaa kichwani hadi leo,”amesema Priscy
Aidha aliongeza kwa kueleza, “Tulikuwa kwenye kama mkusanyiko hivi, watu walikuwa wakicheza, kulikuwa na watu wengi sana… lakini ilikuwa kama ni sisi wawili tu. Hatukumjua mtu mwingine yeyote pale. Na ghafla tu, tulihisi ule muunganiko. Nilijua tu kwamba, “ndiyo, huyu ni mtu maalum.”
Utakumbuka wawili hao walifunga ndoa yao ya kwanza nchini Tanzania Februari 7,2025 huku jana wakifanya harusi nyingine ya kitamaduni nchini Nigeria.

Leave a Reply