Mkali wa Hip-Hop kutoka Marekani, Diddy Combs anakabiliwa na kesi nyingine ya madai ya unyanyasaji wa kingono yanayodaiwa kufanyika mwaka 2000.
Kwa mujibu wa hati zilizopatikana na TMZ mwanamke huyo ambaye jina lake halijawekwa wazi ameeleza kuwa alifanyiwa unyanyuasaji wa kingono na Diddy pamoja na washirika wake wawili alipokuwa na umri wa miaka 16.
Aidha alieleza kuwa Diddy na wenzake walimpa ofa ya kumpeleka nyumbani, na baada ya kushinikizwa alikubali kwa shingo upande lakini alihisi hofu ndipo Combs akampa kinywaji kilichomfanya ahisi kizunguzungu na baada ya hapo Diddy alidaiwa kumbaka na kumtelekeza kwenye moja ya ukumbi wa jengo lake.
Hata hivyo kufuatia na kesi hiyo timu ya wanasheria wa Diddy imejibu madai haya mapya ikimtetea rapa huyo kuwa hajawahi kufanya unyanyasaji wa kingono kwa mtu yoyote.
“Haijalishi ni kesi ngapi zinaletwa, haitabadilisha ukweli kwamba Bw. Combs hajawahi kumdhalilisha kingono au kufanya biashara ya ngono na mtu yeyote mwanaume au mwanamke, mtu mzima au mtoto.
Tunaishi katika dunia ambapo mtu yeyote anaweza kufungua kesi kwa sababu yoyote ile. Kwa bahati nzuri, kuna mchakato wa haki na usio na upendeleo wa mahakama wa kutafuta ukweli, na Bw. Combs ana imani kwamba ataibuka mshindi mahakamani,” wameeleza timu ya wanasheria wa Diddy
Utakumbuka kuwa Combs alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16,2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo, akikabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025. Kwa sasa rapa huyo amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn.
Leave a Reply