Usiku wa kuamkia leo Desemba 15, 2024 mitandao ya kijamii imechafuka picha na video za mwanamuziki wa Marekani Chris Brown, kufuatia onesho alilofanya Afrika Kusini kujaza uwanja wa FNB Stadium wenye uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 94,736.
Mkali huyo kwa sasa yupo kwenye ratiba ya kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kwa ajili ya onesho la Albamu yake mpya inayoitwa 11:11 iliyoachiwa Novemba 23,2023 huku ikifanya vizuri katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali na kumuweka kwenye nafasi nzuri za kimuziki duniani.
Mapema mwaka huu Brezzy alitangaza onesho hilo ambalo lilipewa jina la 'Chris Brown Live In Johannesburg' lililopangwa kufanyika siku mbili mfululizo, Desemba 14, na leo Desemba 15, 2024 .
Utakumbuka tiketi zote za show hiyo ziliisha ndani ya saa 2 muda mchache baada ya kutangazwa. Hii inakuwa ni mara nyingine kwa Breezy kufanya show kubwa S.A baada ya miaka 9 iliyopita ambapo alitumbuiza katika uwanja wa Coca Cola Dome.
Hata hivyo licha ya wanaharakati na vikundi vya utetezi wa haki za binadamu nchini humo kama 'Women For Change"' na chama cha siasa 'GOOD' kutaka mwimbaji huyo kuzuiwa kufanya tamasha hilo S.A kutokana na historia yake ya unyanyasaji na kukutwa na hatia ya ukatili wa kijinsia, tamasha hilo bado litaendelea huku likikadiliwa kuingiza mashabiki zaidi ya 94,736.
Tiketi za levo ya juu kwenye onesho hilo zilikuwa zikiuzwa kwa gharama ya laki 9 kwa tiketi moja na za levo ya chini ziliuzwa kwa 94000 na zote ziliisha ndani ya saa 2.
Leave a Reply