Baba Wa Rihanna Azikwa Mwezi Mmoja Baada Kifo Chake

Baba Wa Rihanna Azikwa Mwezi Mmoja Baada Kifo Chake

Baba mzazi wa mwanamuziki wa Marekani Rihanna, Ronald Fenty, amezikwa jana Jumanne, Julai 8, 2025 nyumbani kwao Barbados baada ya kufariki Mei 31,2025.

Rihanna na baba watoto wake A$AP Rocky walikuwa miongoni mwa waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho na kushiriki ibada ya mazishi ya mzee Fenty iliyofanyika katika ukumbi wa Garfield Sobers Gymnasium huko Barbados, Caribbean.

Ronald alifariki Mei 31, 2025, akiwa na miaka 70 katika Hospitali ya Cedars-Sinai, jijini Los Angeles, Marekani, ambako alilazwa kwa matibabu. Ameacha watoto sita, akiwemo Rihanna, wajukuu 10 na vitukuu.

Sababu ya mwili wake kucheleweshwa kuzikwa ni kutokana na tamaduni za watu wa maeneo ya Carribean, lakini pia uchunguzi wa wataalamu wa afya ambao mwezi mmoja baada ya kufariki kwake walibainisha kuwa kifo chake kilitokana na maradhi ya nimonia, saratani ya kongosho na figo kufeli.

Kifo cha Fenty kimetokea wakati Rihanna akiwa mjamzito akitarajia kupata mtoto wa tatu na mpenzi wake A$AP Rocky.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags