Ayra Starr ajitosa kwa Jay Z

Ayra Starr ajitosa kwa Jay Z

Mwanamuziki wa Afrobeat kutokea Nigeria Ayra Starr anadaiwa kuingia mkataba wa kimataifa na kampuni ya burudani Roc Nation inayomilikiwa na rapa Jay Z.

Mwimbaji huyo anadaiwa kusaini mkataba huo kwani jina lake na picha yake sasa inapatikana kwenye tovuti rasmi ya Roc Nation.

Haya yanajiri wiki kadhaa baada ya Roc Nation kumpongeza Ayra baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza ya BET, ambayo wengi waliona kama ishara ya mapema ya ushirikiano wao.

Hata hivyo, siku nne zilizopita Ayra Starr aliachia kionjo cha wimbo wake ujao 'Hot Body' ambao unatarajiwa kuachiwa chini ya usimamizi wa Roc Nation.

Ingawa hakuna taarifa rasmi zinazothibitisha Ayra kujiunga na kampuni ya Roc Nation, lakini dalili zinaonyesha msanii huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye bado amesainiwa na Mavin Records ya Nigeria ameanza pia kusimamiwa na kampuni ya kimataifa ya burudani ya Jay-Z, Roc Nation.

Ayra Starr anaungana na vinara wengine wa muziki Nigeria ambao wanashirikiana na Roc Nation, akiwemo Tiwa Savage mwaka 2016, Wizkid 2016, na Burna Boy 2017.

Kwanini imekuwa rahisi Ayra Starr kufanya kazi na Roc Nation

Februari 26, 2024, kampuni kubwa ya muziki ya UMG's 'Universal Music Group' ilitangaza kununua hisa kwenye lebo ya Mavin Record na kuchukua majukumu ya kutangaza wasanii wa lebo hiyo nje ya Afrika.

Utakumbuka, kampuni ya burudani ya Jay-Z, Roc Nation, ina ushirikiano wa miaka mingi na Universal Music Group (UMG) ambayo hushirikiana pia na Mavin Records. Ushirikiano huu, uliotangazwa mwaka wa 2013, unaruhusu Roc Nation kufanya kazi kama lebo inayojitegemea ndani ya UMG.

Muziki wa Jay-Z, pamoja na ule wa wasanii wengine wa Roc Nation kama Rihanna, unasambazwa kupitia UMG. Hivyo imekuwa rahisi kwa Roc Nation kufanya kazi na Ayra kutokea Mavin Record kwa sababu lebo hizi tatu zinaushirikiano.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags