Abigail, Harmonize waendelea kukimbiza

Abigail, Harmonize waendelea kukimbiza

Ni Bongo Fleva tena kwenye ramani ya muziki duniani na sasa ngoma ya 'Me Too' ya kwao Abigail Chams na Harmonize imechezwa kwenye Official UKChart Show ya kituo cha habari cha BBC Radio 1Xtra kilichopo Uingereza.

Abbychams ameelezea furaha yake baada ya tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema tukio hilo ni muhimu na halitosahaulika kwake.

"Haya ni matukio muhimu ambayo daima yatawekwa chapa katika moyo wangu"

Ngoma hiyo ambayo iliachiwa Februari 27, 2027 ikiwahusisha wakali hao wa Bongo Fleva imefanikiwa kuongoza chati mbalimbali za muziki nchi za Afrika Mashariki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags