Birthday ya Rais Samia gumzo mtandaoni

Birthday ya Rais Samia gumzo mtandaoni

Ikiwa imetimia takriban miezi sita tangu Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo ni siku yake ya kuzaliwa na ametimiza umri wa miaka 62.

Samia aliapishwa rasmi kuwa Rais wa Tanzania Machi 19, 2021 hivyo kuwa Rais wa kwanza mwanamke tangu Uhuru wa Tanganyika na pia katika ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kufariki dunia Rais John Magufuli.

Wakati leo akisheherekea siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa, viongozi mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamejitokeza kumtakia heri ya siku hiyo na kumuombea maisha marefu yenye baraka tele.

Baadhi ya viongozi hao ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Fedha na Mipango Mwingulu Nchemba, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Mawaziri wote hao katika ukurasa zao za Twitter na Instagram wameandika maneno ya kumtakia heri na afya njema Rais Samia ili aendelee kutekeleza kazi ya kuwatumikia watanzania.

Mbali na viongozi wa juu wa Serikali, heri ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia imetolewa pia na mashirikia mbalimbali ya watu binafsi na serikali pamoja na wananchi wa kawaida katika kurasa zao.

Ndio unaweza kusema leo Rais Samia amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kwa maana kila kona kila mahali watu wameendelea kumtakia heri na kumuandikia maneno ya faraja.

Kwa Rais Samia anasherehekea siku yake hiyo akiwa tayari ametoa uongozi kwa wanawake wengi hasa katika nafasi za maamuzi na akiwa anatimiza miaka 62 leo anajivunia kutekeleza vizuri azimio la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) la maendeleo na usawa la mwaka 2008.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags