Billinass aweka wazi jinsia ya mwanae

Billinass aweka wazi jinsia ya mwanae

Na Habiba Mohamed

Aloooooooh! Baada ya kuficha kwa muda mrefu kuwa nandy hajajifungua mara hatotaja jinsia wala jina la mtoto, waswahili wenyewe wanasemaga ni maneno ya mimba tuu na wala hawakuongopa, basi bwana baba mtoto leo ameweka wazi jinsia ya mtoto wake na kushusha ujumbe mzito kwa mkewe na binti yake.




Billinass kupitia ukurasa wake huku akiambatanisha na video akiwa yeye mkewe na mtoto wao wa kike na kuandika kuwa “Ahsante Mungu Kwa zawadi na Barak, kila iitwapo leo!! Kwangu Mimi 2022 ni Mwaka wa kipekee sana nina kila sababu ya kushukuru na Kutoa Sadaka Mungu Wetu ni Mwema Sana” aliendelea kwa kuandika

“Pili Niseme Ahsante Mke wangu Kipenzi Nandy Kwa Kuniletea Mrembo na Rafiki, Haikuwa Kazi Rahisi umenionesha wewe ni Shujaa kiasi gani kwanzia Mtoto akiwa tumboni mpaka Muda unajifungua umepigana sana  nimejionea namna gani mtu anaweza kurisk kupoteza uhai wake wakati wa kujifungua Hii imefanya nizidi kukupenda, Kukuheshimu na kukupa Nafasi ya Pekee katika Maisha Yangu” ameandika Billnenga

Bwana bwana baba wa mtoto ameamua kweli kweli hakuishia hapo aliendelea kwa kuandika “Hayo Yote Hayatoshi Lakini Kila Siku Nakuombea Kwa Mungu akulinde Mke Wangu na Nitakupa Furaha Na Kufanya Maisha Yako Yawe ya Amani kwani Unastahili Mengi Mazuri sina zawadi kubwa itakayoweza lingana na Upendo wangu kwako zaidi ya kuzidisha upendo kila iitwapo leo, Tatu kwa Mwanangu kipenzi Najuwa ipo siku utakuja kuisoma Hii Niseme tu Nakupenda Sana sana na Umekuja na Baraka Nyingi ambazo siwezi hata kuzielezea Mwenyezi Mungu akutunze ukawe mtu mwema wa kawaida na kiroho pia nikupongeze kwa kuwa balozi” ameandika Billnass






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags