Biden kukutana na Xi Jinping huko Bali, Indonesia

Biden kukutana na Xi Jinping huko Bali, Indonesia

Rais wa Marekani Joe Biden, leo anakutana na Xi Jinping wa China huko Bali, Indonesia kwa ajili ya kujadili mahusiano kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani wakati wanapopigania ushawishi wa kimataifa.

Mkutano huu unaofanyika pembezoni mwa mkutano wa nchi ishirini zilizoendelea na zinazoendelea kiviwanda G20, ndio wa kwanza kwa viongozi hao wawili kukutana ana kwa ana tangu Biden alipochukua hatamu za uongozi Marekani.

Uhasama kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu duniani umezidi wakati ambapo China inazidi kuwa na ushawishi. Biden anatarajiwa kuishinikiza China kuingilia kati hatua ya rafiki yake Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia wakati ambapo kuna hofu kwamba huenda kiongozi wake Jim Jong Un akafanya jaribio lake la saba la kombora la nyuklia.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags