Baba Levo: Nitahakikisha Diamond anamuoa Zuchu

Baba Levo: Nitahakikisha Diamond anamuoa Zuchu

Aloooooh! Kwahiyo huu mwaka tutakula ubwabwa wa shughuli mpaka basi, naona watu wamejipanga haswaaa, basi bwana chawa kama chawa Baba Levo amewaaminisha watu kuwa atafanya kila awezalo Mondi amuoe dada Zuhura.

Baba Levo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe akiwa ameambatanisha picha ya boss wake Diamond na zuchu ujumbe huo ukiwa unaeleza kuwa, “Nitahakikisha Diamond anamuoa Zuchu, hakuna mambo ya mchezo mchezo hapa, hii ni atake asitake atamuoa,” ameandika Baba Levo.

Uwiiiih! Haya wafuatiliaji wa Mwananchi Scoop je chawa huyu mkubwa kabisa ataweza kufanikisha hili, embu dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags