Azimia kwa kulipa kodi miaka 15 nyumbani kwa mkewe

Azimia kwa kulipa kodi miaka 15 nyumbani kwa mkewe

Ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, yamemkuta Mwanaume mmoja huko nchini Zambia amejikuta anapoteza fahamu baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye mwenye nyumba aliyokuwa analipia kodi kwa miaka 15.


Nyieee hahaha wanawake mnasiri kubwa daah,Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Martin Stampa amepata na maswahibu hayo baada ya kumtambia mke wake kuwa anatafuta mwanamke mwengine mwenye akili na atakaye mpa mawazo ya kimaendeleo zaidi (kuliko mke wake)


Baada ya kauli hiyo mke wake akamwambia kuwa yeye ndiye hana akili maana amekaa kwenye nyumba hiyo kwa miaka 15 akilipa kodi zaidi ya Laki 5 kwa mwezi bila kugundua kuwa alikua anamlipa mke wake (mmiliki wa nyumba).

Unaambiwa kwa miaka yote hiyo mzee baba Stampa alikua akimkabidhi mke wake pesa ili alipe kodi kwa mwenye nyumba kumbe nyumba ni ya mke wake.

Taarifa hiyo ilimshtua sana Stampa jambo ambalo lilipelekea apoteze fahamu.

Daaaah wanaume nahitaji comment zenu hapa juu ya hili nyieeee wanawake mtakuja kuwaua wenza wenu hahaha.






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags