Amkataa mama yake ataka kuishi na Tyrese

Amkataa mama yake ataka kuishi na Tyrese

Binti wa mwanamuziki na mwigizaji Tyrese Gibson, Shayla (18), amkataa mama yake aitwaye Norma Mitchell na kwenda kuishi kwa baba yake huku akishusha lawama kwa mama huyo.

Katika moja ya mahojiano binti huyo alisema licha ya kuwa mama yake amekuwa akijaribu kuwatenganisha, lakini uhusiano wake na baba yake ulizidi kuimarika alipogundua kuwa hana hatia kama alivyokuwa akielezwa na mama yake.

Ikumbukwe Tyrese na Norma walifunga ndoa 2007 na kutalikiana 2009 ambapo 2017 waliingia makubaliano ya pande zote mbili kumlea mtoto wao kwa kushirikiana.

Kutokana na hayo hatimaye Tyrese, ambaye amekuwa akiweka wazi kuhusu changamoto zake, sasa anapata faraja kwa kujenga upya uhusiano wake na binti yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags