Aliyekuwa mkwe wa Bob Marley atunukiwa tuzo na Apple music

Aliyekuwa mkwe wa Bob Marley atunukiwa tuzo na Apple music

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani ambaye pia alikuwa mpenzi wa mtoto wa Bob Marley, Rohan Marley, Lauryn Hill ametunukiwa tuzo ya heshima na ‘Apple Music’ baada ya albumu yake ya ‘The Miseducation of Lauryn Hill’ ya mwaka 1998 kushika namba 1 kati ya albumu bora 100 za kale.

Siku ya jana Jumatano, Mei 22, Apple Music ilimualika Hill katika ghafla ya kumkabizi tuzo hiyo iliyofanyika New York City ambapo Albamu hiyo ya Hill ilizipiku albumu nyingine za zamani kutoka kwa wasanii kama Beyoncé, The Beatles, Michael Jackson, Prince, Stevie Wonder, Kendrick Lamar, Amy Winehouse, Frank Ocean na Nirvana.

Lauryn Hill na Rohan Marley walikutana mwaka 1996 na kuanzisha uhusiano, wawili hao walibahatika kupata watoto watano na kuripotiwa kuachana mwaka 2008.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags