Aina ya vyakula ambavyo ukivichanganya pamoja havina faida kwenye mwili

Aina ya vyakula ambavyo ukivichanganya pamoja havina faida kwenye mwili

Haya haya!! Wapenda afya wenzangu tumerudi tena kwa hewa bwana kama mnavyojua matumizi ya aina mbalimbali ya vyakula katika jamii za Kiafrika hususani nchini Tanzania limekuwa ni jambo la kawaida, kwani wengi wetu hutumia vyakula hivyo bila kujua madhara gani yanaweza kujitokeza endapo vyakula hivyo vikichanganywa.  

Nchini Tanzania hususani katika migahawa mbalimbali wauzaji wa vyakula wamekuwa na tabia ya kupika vyakula vya aina tofauti tofauti huku wakivichanganya pamoja bila ya kujua mchanganyiko wa baadhi ya vyakula huweza kuleta changamoto katika mwili wa binadamu.

Mwananchi Scoop tumekuangazia na kukuletea aina ya vyakula ambavyo huwa vikichanganywa pamoja huweza kuleta madhara katika mwili wa mwanadamu, utafiti kutoka kwa wataalamu na tovuti mbalimbali.

Tovuti ya india.com inaeleza kuwa kuna aina ya vyakula vikichanganywa huleta madhara katika mwili wa binadamu na haishauriwi kwa vyakula hivyo kutumiwa kwa wakati mmoja.

Mayai na Nyama ya Nguruwe kitaalamu hivi haviruhusiwi kutumika kwa wakati mmoja, kwani endapo mtu atatumia kwa kula basi anaweza kupata changamoto ya kiafya.

Vyakula hivi viwili vina protini nyingi na huwa vizito katika tumbo hivyo itachukua muda mrefu kusaga vyakula vyote viwili, hivyo mtu anashauriwa kula protini nyepesi kwanza na kisha nyama

Hata hivyo matumizi ya Sharubati itokanayo na machungwa pamoja na matumizi ya maziwa havitakiwi kutumika kwa pamoja kwani maziwa huchukua muda kumeng’enywa mwilini.

Unapotumia maziwa na matunda ya machungwa pamoja, maziwa huganda, hii inaweza kusababisha kujaa kwa gesi tumboni.

Chakula cha jibini na kinywaji baridi, muunganiko huu huleta madhara katika mwili wa binadamu kwani mchanganyiko unaweza kusababisha usumbufu na maumivu ya tumbo.

Kwa upande wao tovuti ya “Health” inasema endapo baadhi ya vyakula kama ndizi na maziwa, nyama na viazi vinaweza kuleta madhara endapo vikitumiwa mara kwa mara.

Mfano matumizi ya viazi na nyama kwa wakati mmoja huweza kupelekea matatizo ya umeng’enyaji chakula au matatizo ya tumbo.

Akizungumza na Mwananchi mtaalam wa lishe Sweetbert Njuu alisema chakula kama nyama na maziwa havitakiwi kutumiwa pamoja kwani mtu hataweza kupata faida ya vyote vikitumika pamoja.

“Vyakula hivi vinashauriwa angalau vipishane lisaa limoja endapo mtu ata tumia, kwa sababu madini ya chuma na madini ya kalsiamu yanakinzana” alisema Njuu

Alisema matumizi ya pombe upelekea ufanisi mbaya wa ufyonzaji wa chakula mwilini, hivyo pombe haishauriwi kutumiwa endapo mtu anakula chakula.

“Ikiwa mtu amekunywa pombe nyingi sana na wakati huo huo amekula chakula chenye sifa ya mlo kamili basi uwezekano wa ufyonzaji chakula unaweza kufika asilimia 50” alisema Njuu

Hata hivyo matumizi ya matunda na nafaka zisizo kobolewa kwa wakati mmoja kitaalamu huweza kusababisha baadhi ya changamoto katika tumbo, mfano tumbo kujaa gesi

Sweetbert Njuu alisema watu wanatakiwa kuzingatia matumizi ya lishe bora ambayo, huwa na mboga mboga, matunda, nafaka zisizo kobolewa, vyakula vitokanayo na mizizi, matumizi ya protini nzuri, yani nyama zisizo na mafuta na bila kusahau kunywa maji ya kutosha.

Mtaalamu wa lishe kutoka Mloganzila Theresia Thomas alisema matumizi ya Kahawa yenye Kafeini na vyakula vyenye madini chuma kama nyama, mtumiaji anaweza kupata tatizo la upungufu wa damu.

“Kafeini inaenda kuzuia ufyonzwaji wa madini chuma hivyo kumfanya mtumiaji kukosa madini chuma mwilini,na humpelekea kuwa na upingufu wa damu” alisema Theresia.

Hata hivyo alisema endapo vyakula vyenye kalsiamu vikichanganyawa pamoja na vile vya madini chuma kama vyakula vyenye kalsiamu vikizidi basi inaweza kuleta changamoto ya kiafya.

“Mfano ndio maana tunashauri watoto wadogo wasipewe maziwa ya Ng’ombe, kwa sababu humpa kalsiamu kwa wingi na kuzuia upatikanaji wa madini chuma” alisema Theresia.

Pamoja na hayo, Shirika la Afya Duniani (WHO) Juni 7, 2022 walizungumzia umakini na kuhamasisha hatua za kuzuia, kugundua na kudhibiti hatari zinazotokana na chakula na kuboresha afya ya binadamu

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post