Ahukumiwa kuswali swala tano kwa siku 21

Ahukumiwa kuswali swala tano kwa siku 21

Mahakama katika mji wa Malegaon katika jimbo la Maharashtra nchini Indi,a imemuamuru mshtakiwa kusali swala tano kwa siku, kwa siku 21 zijazo ili kumuadhibu kwa kupigana.

Uamuzi wa Jaji Tejwant Singh Sindhu pia uliamuru mshtakiwa Rauf Umar Khan mwenye umri wa miaka 30 kupanda miti miwili karibu na msikiti ili kumuondolea kesi hiyo ya uhalifu wake na kutunza miti hiyo miwili.

Aidha hakimu huyo alimkuta mwanamume huyu na hatia ya kumjeruhi mwenzake katika mgogoro wa mtaani.

Hakimu ambae sio muislamu, pia alimuamuru afisa kilimo wa wilaya hiyo kufuatilia utekelezaji wa amri ya mahakama na kumruhusu kutumia jeshi la polisi ikibidi kutekeleza agizo hilo.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post