Afya ya bondia Coleman yazidi kuimarika

Afya ya bondia Coleman yazidi kuimarika

Baada ya kuripotiwa kuwa katika hali mbaya kutokana na kunusurika kwenye ajali ya moto, familia ya bingwa wa zamani wa UFC Mark Coleman, imeripoti kuwa mkali huyo kwa sasa anaendelea vizuri.

Taarifa hiyo imetolewa na watoto wa bondia huyo kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo walichapisha video wakiwa na baba yao ambaye bado anapumulia mipira.

Ikumbukwe kuwa Mark Coleman alikimbizwa hospitali na ndege baada ya kunusurika katika ajali ya moto wakati alipokwenda kuwaokoa wazazi wake Dan na Connie Foos Coleman kwenye moto ambao ulizuka katika nyumba yao.

Mark alijitokeza kwa mara ya kwanza katika eneo la michezo mchanganyiko ya kijeshi (MMA) mwaka wa 1996. Alinyakua mataji ya ubingwa wa uzito wa juu katika UFC mara 10 na #UFC 11, aidha aliripoti kustaafu 2013.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags