Rio de Janeiro jaji kutokea nchini Brazil, ameamuru kufutwa kwa wimbo wa 'Million Years Ago' wa mwimbaji wa Uingereza Adele kutokana na madai ya wizi wa kazi hiyo kutoka kwa mwanamuziki wa Brazil anayefahamika kama Toninho Geraes.
Uamuzi huo uliotangazwa hadharani Desemba 16, 2024 ulikuja baada kesi iliyowasilishwa mwaka huu na Toninho Geraes ambaye anadai Adele aliiga wimbo wake uliotoka miaka ya 1990 unaofahamika kama 'Mulheres'.
Kutokana na hilo wameamuru makampuni yanayomsimamia Adele ambayo ni 'Sony Music Entertainment' na 'Universal Music' kuondoa wimbo huo kwenye majukwaa yote ya kuuzia na kusikilizia muziki na itawalazimu kulipa faini ya USD 8,080.94 sawa na Sh 19 milioni ikiwa kampuni hizo zitashindwa kutii agizo hilo.
Hata hivyo, Universal ilikata rufaa dhidi ya madai hayo Jumanne Desemba 17, ikisema hakuna wizi bali ni "kufanana kwa sauti kwa bahati mbaya,"
Adele na Geraes wote wanamikataba na Universal, lakini mwanamuziki huyo wa Brazil amekuwa akijaribu kusitisha mkataba wake na kampuni hiyo kutokana na madai yake ya wizi, wakili wake alisema.
Wimbo wa 'Million Years Ago' ulitoka Desemba 21, 2019 ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 22 kwenye mtandao wa YouTube.
Leave a Reply