50 Cent: Lamar amestahili kupiga show Super Bowl

50 Cent: Lamar amestahili kupiga show Super Bowl

‘Rapa’ 50 Cent anadai kuwa msanii Kendrick Lamar, amestahili kuchaguliwa kuongoza show ya Super Bowl Halftime inayotarajiwa kufanyika Februari mwaka 2025 jijini New Orleans.

Wakati alipokuwa kwenye mahijiano yake katika kipindi cha ‘The Talk’ waandishi walimuuliza 50 kuhusiana na mtazamo wake kuhusu Super Bowl, Cent anadai kuwa anamuamini Lamar na alistahili kuchaguliwa kutumbuiza katika tamasha hilo.

“Naamini, ilikuwa ni chaguo sahihi. Kama msanii wa peke yake kwa sasa, yeye ndiye anayetikisa kwenye tasnia ya muziki, kwahiyo amestahili” amesema 50 Cent

Aidha alizungumzia kuhusu mzozo wa Kendrick Lamar kuchaguliwa kufanya show New Orleans badala ya mzawa na gwiji wa rap kutoka NOLA, Lil Wayne, 50 Cent kwa upande wake anadhani kuwa Wayne asingekuwa mwongozaji mzuri katika tamasha hilo, huku akimshauri Lamar awaalike baadhi ya washirika wenzake wa zamani akiwemo Dr. Dre ili show yake iweze kubamba.

Hata hivyo aligusia kidogo kuhusu ugomvi kati ya Kendrick Lamar na Drake, 50 Cent ambapo alidai kuwa ugomvi wa wawili hao ulikuwa ni mzuri kwani uliwafanya wasanii hao kuchangamsha vichwa kwa kuandika nyimbo pamoja na kuufanya muziki wa Hip hop kuwa juu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags