ZUCHU: Msanii akiolewa au kujifungua tumempoteza kwenye game

ZUCHU: Msanii akiolewa au kujifungua tumempoteza kwenye game

Na Habiba Mohamed

Waswahili walisema mshika mawili Moja humponyoka..Ebwaaana kunako mitandao ya kijamii hivi karibuni zilitembea sana picha na video za harusi za mastaa wawili  Nandy na Billnass na baadhi ya wasanii walipost Kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kuwapongeza wawili hao Ila baadhi ya wasanii walikuwa na mtazamo wa tofauti kuhusu msanii Nandy kuolewa na hata kubeba ujauzito.


                                               ZUCHU

Msanii zuchu moja kati ya mahojiano aliyoyafanya na kituo kikubwa cha habari alizungumza yafuatayo kuhusiana na ndoa ya Nandy akisema, "Msanii yeyote wa kike kuwaza kuolewa sio jambo muhimu kwasababu muziki unahitaji muda na kujitoa sana. Nandy kuolewa na kubeba ujauzito, hongera kwake maana ni ujasiri ameonesha tena kwa msanii mkubwa kama yeye."


                                           NANDY

Kauli hiyo ya msanii Zuchu inaturudisha nyuma kidogo kwa wasanii wa kike wa mziki wa Bongo Fleva kama Vanessa Mdee ambaye aliamua kujing'amua kutoka kwenye tasnia ya mziki baada ya kuingia kwenye mahusiano na muigizaji Rotimi, vilevile msanii Shaa ambaye pia amepotea kwenye game la mUziki wa Bongo fFeva baada ya kuingia kwenye uhusiano na ulezi wa mtoto wake aliyezaa na Master J na wasanii wengine kama Marissa.

   
                                         VANESSA                                                                                                        SHAA

Hii inatoshaa kusema mahusiano, ndoa au uzazi unachangia kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wasanii kuacha vipaji vyao kwasababu ya majukumu kuongezeka na wengine kuendelea kupambania nafasi zao katika tasnia ya mziki licha ya majukumu ya ndoa au ulezi waliyonayo mfano Ruby na Aika.

  
                                                        AIKA

Let me know your comments below ...kipi kifanyie Ili wasanii wakike waendele kumaintain kwenye tasnia ya mziki licha ya majukumu ya ndoa,mahusiano na uzazi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags