Zuchu aomba radhi kwa jamii

Zuchu aomba radhi kwa jamii

Baada ya kuomba radhi kupitia ‘Lebo’ yake ya WCB kufuatiwa na kutumia lugha isiyofaa katika show yake ya Fullmoon Kendwa Visiwani Zanzibar na kupelekea kufungiwa kujishughulisha na shughuli za Sanaa Zanzibari, na sasa Zuchu ameomba radhi kwa jamii.

Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram ameomba radhi kwa kitendo kilichotokea huku akieleza kuwa haikuwa kusudio lake kusema maneno yale kwani lengo lake lilikuwa ni kuburudisha na sio kupotosha umma.

Hata hivyo amelishukuru Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kumuita ofisini kwao na kumpa maelekezo pamoja na muongozo wa maadili katika kazi ya Sanaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags