ZENA MAYEYE: MISS IFM 2022

ZENA MAYEYE: MISS IFM 2022

Aloooooh! Nawasalimu kwa jina la miss IFM huhuhu! Leo bwana kwenye ile segment yetu pendwa ya UNICORNER ambayo tunakupa burudani na mambo yote yanayojiri katika vyuo vikuu, tumekuja na jipyaaaa. Basi bwana sie tena katika pitapita zetu tukakutana na vibe sio poa la mashindano ya Miss katika chuo cha usimamizi wa fedha  - IFM.

Shindano hilo lilifanyika week hii July 23, ambapo lilifanyika kwenye barabara inayotengenisha chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa Posta.

Aidha katika mashindano hayo Zena Mayeye, mwenye umri wa miaka 20, ambae anachukua kozi ya BAC1,  ameibuka kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha Miss IFM 2022/23 baada ya kuwagaragaza wenzake katika fainali za mashindano hayo yaliyofanyika katika chuo hicho, Posta, Dar Es Salaam.

Usiache kudondosha komenti yako hapo chini na kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa stori mbalimbali @Mwananchiscoop.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post