Zambia yataka majibu kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyefariki Ukraine kwa mazingira ya kutatanisha

Zambia yataka majibu kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyefariki Ukraine kwa mazingira ya kutatanisha

Zambia imetaka majibu kuhusu kifo cha mwanafunzi Lemekhani Nyirenda, aliyefariki nchini Ukraine kwa mazingira ya kutatanisha.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23, mwanafunzi katika Taasisi ya Fizikia ya Uhandisi ya Moscow, alikuwa anatumikia kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la kutumia dawa za kulevya.

Alifariki mwezi Septemba lakini Urusi ndiyo kwanza imeiarifu serikali ya Zambia.

Ubalozi wa Zambia nchini Urusi uligundua kuwa mwili wa Bw Nyirenda tangu wakati huo ulikuwa umesafirishwa hadi mji wa mpakani wa kusini mwa Urusi wa Rostov-on-Don ukiwa tayari kurejeshwa Zambia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Stanley Kakubo alisema.

Zambia imezoea kupeleka wanafunzi nchini Urusi kwa ufadhili wa masomo, kama ilivyokuwa kwa Bw.Nyirenda.

Mazingira ya kuachiliwa kwake kutoka gerezani hayajulikani, lakini Urusi imetoa uhuru kwa baadhi ya wafungwa ikiwa watapigana katika vita vyake nchini Ukraine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags