Zaidi ya  watu 400 hawajulikani walipo kufuatia kimbunga freddy

Zaidi ya watu 400 hawajulikani walipo kufuatia kimbunga freddy

Mamlaka nchini Malawi zinasema idadi ya watu ambao bado hawajulikani walipo kufuatia kimbunga Freddy imeongezeka kutoka 349 hadi 427, huku nchi nyingi zikiendelea kutuma misaada ya kibinadamu.

Idara ya masuala ya kukabiliana na majanga ya Malawi (DoDMA), siku ya Jumatatu ilisema ilipokea ripoti za tathmini ya haraka kutoka mikoa 15 iliyoathirika nchini humo.

Mpaka kufikia Jumatatu, Machi 20, 2023, idadi ya watu waliokimbia makazi yao ni 508,244, huku idadi ya vifo ikiongezeka kutoka 476 hadi 499, na majeruhi 1,332. Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Tanzania na Zambia zimetuma timu kusaidia katika shughuli za uokoaji.

Dhoruba hiyo ilipiga Msumbiji na Malawi wiki iliopita kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja, na kuharibu nyumba nyingi na kusababisha mafuriko makubwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags