Wanajeshi wasiopungua 51 wa Burkina Faso wameuwawa katika shambulizi la kustukiza lililotokea eneo la kaskazini mwa nchi hiyo linalofahamika kwa hujuma kubwa za makundi ya itikadi kali.
Taarifa iliyotolewa jana na jeshi la Burkina Faso imesema wanajeshi hao walishambuliwa kwenye jimbo la Oudalan ambalo linaitenganisha nchi hiyo na taifa jirani la Mali.
Aidha shambulio hilo ambalo linatajwa kuwa limesababisha idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi kwa wakati mmoja tangu kuzuka kwa uasi wa makundi ya itikadi kali nchini humo limetokea siku mbili kabla ya Ufaransa kuhitimisha operesheni zake za kijeshi nchini humo.
Leave a Reply