Yung Miami aegemea upande wa Diddy

Yung Miami aegemea upande wa Diddy

Rapa Yung Miami ambaye pia ni mpenzi wa zamani wa Diddy amedai kuwa wakati yupo na Combs hakuwahi kufanyiwa ukatili wowote.

Yung ameyasema hayo baada ya kuwa na mijadala mingi mitandaoni kuhusiana na video ya Diddy ikimuonesha anampiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie huku baadhi ya wadau wakimtaka ‘rapa’ huyo kueleza kwa upande wake endapo kuna unyanyasaji wowote aliwahi kufanyiwa.

Wakati akiwa kwenye mahojiano na Tmz Yung Miami amesema kipindi yupo kwenye mahusiano na Diddy hakuwahi kufanyiwa matukio ya unyanyasaji na uhusiano wao ulikuwa wa manufaa katika kazi zao za muziki.

Utakumbuka Yung Miami na Diddy walianza uhusiano mwaka 2012 na kutengana April 2023 baada ya Diddy kupata mtoto na mwanamke mwingine huku mpaka kufikia sasa wawili hao wanadaiwa kuwa marafiki tuu wa kusaidiana katika kazi zao.

Ukiachilia hayo mwanadada huyo pia alihusishwa kwenye kesi ya Diddy iliyofunguliwa na Rodney Jones kuwa Yung Miami alikuwa akitumika kwa ajili ya kumbebea madawa ya kulevya Diddy ambayo yalipatikana nyumbani kwa Combs wakati wa msako uliofanywa na FBA wa Marekani.

Mpaka kufikia sasa Diddy ameshafunguliwa kesi nane tofauti tofauti, nyingi zikiwa za unyanyasaji wa kingono lakini mpaka sasa hakuna ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni mwanamuziki huyo huku baadhi ya mastaa akiwemo Suge Knight wakidai kuwa Diddy ni FBI.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags