William Ruto aelekea DRC katika juhudi za kusaka amani

William Ruto aelekea DRC katika juhudi za kusaka amani

Rais wa Kenya William Ruto anaelekea kwenye ziara mjini Kinshasa leo. Ziara hiyo inazingatia juhudi za kurejesha amani katika eneo la mashariki mwa Kongo. Ziara ya Rais wa Kenya inafanyika baada ya ziara ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ambaye amepewa jukumu la kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Kongo kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya atafanya mazungumzo na mwenzake wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi ambapo watajadili juu ya mahusiano ya kibiashara baina ya nchi mbili hizo, ushirikiano wa kikanda na usalama katika eneo la mashariki mwa Kongo kabla ya kuelekea Korea Kusini.

Mapigano yameongezeka mashariki mwa Kongo wakati kundi la waasi la M23 likizidi kuyadhibiti baadi ya maeneo na kuwalazimisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Kenya inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani na wakati huo huo imewapeleka askari wake nchini Kongo kama sehemu ya kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags