WHO: Majaribio ya chanjo  ya ugonjwa wa ebola kuanza hivi karibuni

WHO: Majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa ebola kuanza hivi karibuni

Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa kliniki ya majaribio ya chanjo inayoweza kukabiliana na ugonjwa wa ebola inaweza kuanza kazi ndani ya wiki chache zijazo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Uganda ilitangaza mlipuko wa ebola Septemba 20 mwaka huu na wizara ya afya hadi sasa imethibitisha jumla ya vifo 19 na watu 54 wakiwa wameambukizwa.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya kuenea kwa maambukizi kote nchini humo, kutokana na kutokuwepo kwa chanjo. Ebola, ni homa inayoambatana na kuvuja damu na huenea hasa kwa kugusana na maji maji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na udhaifu mkubwa, maumivu makali ya misuli, kichwa na koo, kutapika, kuharisha na upele.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags