Wema: Sitofanya party tena, ningekaa kimya ningekufa

Wema: Sitofanya party tena, ningekaa kimya ningekufa

Muigizaji Wema Sepetu ameyatoa ya moyoni baada ya kile kilichotokea kwenye birthday party yake, na kueleza kuwa hatokuja kufanya tena sherehe maisha yake yote.

Wema ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza kuwa nia na madhuni yake ni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na ku-enjoy na wapenzi wake ila haikuwa vile alivyotarajia, kwa ufupi shughuli yake iliharibika sana.

Huku akieleza kuwa lengo lake halikutimia licha kujitahidi kufanya kitu kizuri ambacho kingemfurahisha sana katika siku yake ya kuzaliwa hivyo basi anajisikia vibaya sana kwa kuwa hii ndiyo sherehe mbaya zaidi ya kuzaliwa katika maisha yake.

Aidha mrembo huyo alimalizia kwa kueleza kuwa hatokuja kufanya party tena kwenye maisha yake kwa sababu anaumia moyoni, na ilibidi aongee ili aweze kupumua maana angekaa kimya angekufa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags