Wema: Mimi ni mwanamke wa kwanza Tanzania kufikisha 10M followers

Wema: Mimi ni mwanamke wa kwanza Tanzania kufikisha 10M followers

Aloooooh! Wakati wengine wakisherehekea kuendelea kupata kipato na kuendelea kupata mafanikio zaidi lakini bwana kwa madame mwenyewe Wema Sepetu kwa upande wake amefurahishwa sana na kuwa mtanzania wa kwanza kupata wafuasi million 10.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema ameandika ujumbe mzito ukiwa unasema kuwa “Thank You For 10M Followers By The way vipenzi vyangu... Nabaki kuwa wa Kike wa Kwanza Tanzania kufikisha 10M. Basi naombeni kuanzia sasa, Msinishindanishe na mtu jamani,’’ ameandika Wema Sepetu.

Aidha aliendelea kwa kuandika kuwa “Sijawahi kuwa katika mashindano zaidi ya Miss Tanzania 2006... Ataefuata na kunizidi isiwe Battle Basi wapenzi wangu... Tumefikisha 10M Bila nguvu yoyote... Nitumie tu nafasi hii kusema asanteni na nawapenda,” ameandika Madame Wema.

Haya mwenzangu na mie dondsha komenti yako hapo chini mwanangu sana na utueleze wewe una wafuasi wangapi katika akaunti yako ya Instagram au tukuache kidogo hahah!.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post