Wazazi 763 wakamatwa kwa kutowapeleka shuleni wanafunzi waliofaulu

Wazazi 763 wakamatwa kwa kutowapeleka shuleni wanafunzi waliofaulu

Taarifa kutoka Ruvuma ambapo Idadi hiyo imefikiwa baada ya msako wa Nyumba kwa Nyumba uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, kutokana Wanafunzi wengi wa Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza kutoripoti Shuleni

Hata hivyo maeneo mengi Nchini yamekuwa na mwitikio wa kusuasua kwa Wanafunzi waliofaulu kuripoti Shuleni ambapo hadi kufikia Januari 15, 2023 zaidi ya Wanafunzi 700,000 wa Kidato cha Kwanza, hawakuwa wamefika kwenye Shule walizochaguliwa

Licha ya baadhi ya Wanafunzi kudaiwa kujiunga na Shule za Binafsi imeleezwa bado kuna idadi kubwa ya Wanafunzi waliofaulu wamebaki Nyumbani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Wazazi kutotaka Watoto waende Shule.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags