Wawili wakamatwa kufuatia mauaji ya mwanamitindo Edwin

Wawili wakamatwa kufuatia mauaji ya mwanamitindo Edwin

Jeshi la Polisi nchini Kenya limewakamata watu wawili kufuatiwa na mauaji ya Bw Edwin Chiloba, mwanamitindo na mwanaharakati wa LGBTQ.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) pia wamefanikiwa kupata gari lililotumika kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Chebisas, Kaunti ya Uasin Gishu ambapo aliuawa hadi eneo ambapo sanduku la chuma lilipopatikana.

"Gari ambalo lilitumika kusafirisha mwili wa marehemu limezuiliwa huku uchunguzi kuhusu mauaji hayo ukiendelea," Msemaji wa Polisi Resla Onyango aliambia vyombo vya habari.

Kukamatwa huko kunajiri siku moja baada ya Bw Jackton Odhiambo, ambaye ni mpenzi wa Bw Chiloba, kuripotiwa kukiri kumuua mwanamitindo huyo huku kukiwa na madai ya kutokuwa muaminifu.

Aidha watatu hao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Langas, mjini Eldoret.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags