Watu 11 wafariki katika tamasha la Fally Ipupa

Watu 11 wafariki katika tamasha la Fally Ipupa

Watu 11 wamefariki Jumamosi wakiwemo maafisa wawili wa polisi katika mkanyagano kwenye uwanja wa michezo uliokuwa umefurika watu waliokwenda kuhudhuria tamasha la mwanamziki Fally Ipupa mjini Kinshasa.

Uwanja huo ambao ulisheheni kupita kiwango kinachotakiwa ulijazwa na watu 80,000 kwa ajili ya kushuhudia tamasha la mwanamuziki wa Kongo Fally Ipupa, kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa mambo ya ndani. 

Waandishi habari wa Reuters wamefahamisha kwamba baadhi ya mashabiki wengine walijilazimisha kuingia kwenye eneo la watu maalum yaani VIP na maeneo mengine maalum yaliyotengwa katika uwanja huo.

Taarifa ya polisi imeonesha watu 11 wamefariki kutokana na kukosa hewa pamoja na mkanyagano na wengine 7 wamelazwa hospitali kwa mujibu wa tamko lililotolewa na waziri wa mambo ya ndani wa Kongo, Daniel Aelo Okito.

Imeelezwa kwamba awali polisi walitumia gesi ya kutowa machozi katika jitihada ya kuwatawanya watu waliokuwa wakifanya vurugu katika barabara za nje ya uwanja huo ambako watu walikuwa wameshakusanyika kabla ya tamasha hilo la mwanamuziki mzaliwa wa Kinshasa, Fally Ipupa.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post