Watahiniwa 566,840 kufanya mtihani wa  kidato cha Nne leo

Watahiniwa 566,840 kufanya mtihani wa kidato cha Nne leo

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) unafanyika kuanzia leo tarehe 14 Novemba hadi 1 Disemba, 2022 katika jumla ya Shule za Sekondari 5,212 na Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 1,794.

Jumla ya Watahiniwa 566,840 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2022 ambapo kati yao Watahiniwa wa Shule ni 535,001 na Watahiniwa wa Kujitegemea ni 31,839.

Kati ya Watahiniwa wa Shule 535,001 waliosajiliwa, Wavulana ni 247.131 sawa na asilimia 46.19 na Wasichana ni 287,870 sawa na
asilimia 53.81.

Aidha, wapo Watahiniwa wenye mahitaji maalum 852 na kati yao, 480 ni wenye uoni hafifu, 62 ni wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia, 152 ni wenye mtindio wa akili na 139 ni wenye ulemavu wa viungo ya mwili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post