Wasanii wa Bongo wapata madini kutoka kwa mwigizaji Son Ye-jin

Wasanii wa Bongo wapata madini kutoka kwa mwigizaji Son Ye-jin

Waigizaji wa filamu Tanzania ambao wapo kwenye ziara nchini Korea kwa ajili ya kujifunza masuala ya filamu mapema siku ya leo walikutana na staa wa filamu Korea, Son Ye-jin na kubadilishana mawazo, na kujuzana kuhusu mambo mazima ya filamu.

Aidha kwa mujibu wa mastaa hao wa filamu Tanzania kupitia kurasa zao za Instagram wameweka wazi kuwa sio kukutana tu na Son Ye-jin pia alifanikiwa kuzungumza na watengenezaji wa filamu kotoka nchini humo Cheol-ha Lee na Yohwan KIM.

Kupitia ukurasa wa Idris Sultan ameandika “Ni hisia ya ajabu kukutana na mwigizaji wako wa Kikorea unayempenda @yejinhand, Weeee mama Samia wewee hapa umenikamataaa"

Utakumbuka kuwa wasanii wa filamu Tanzania wapo Korea kwa takribani siku ya nne sasa katika ziara yao ya kujifunza mambo ya filamu.

Baadhi ya mastaa waliyopo kwenye ziara hiyo ni Irene Paul, Wema Sepetu, Idris Sultani, Dorah, Johari Chagula, Steve Nyerere, Eliud Samwel, Getrude Mwita, Gabo Zigamba na Godliver Gordian.

Mwigizaji Son Ye-jin amewahi kuonekana katika filamu kama ‘Blood and Ties’, ‘Spellbound’, ‘The Truth Beneath’ ‘The Last Princess’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags