Wanandoa wahukumiwa miaka minne kwa kuiba mvinyo

Wanandoa wahukumiwa miaka minne kwa kuiba mvinyo

Aliyekuwa malkia wa urembo wa Mexico, Priscila Guevara pamoja na mpenzi wake Consantin Dumitru wahukumiwa kifungo cha miaka minne nchini Uhispania kwa kuiba chupa 45 za mvinyo zenye thamani ya takriban $1.7m.

Tukio hilo lilitokea mnamo mwaka 2021 katika hoteli ya kifahari katika jiji la Uhispania la Cáceres, ambapo wanandoa hao walikwenda kama wageni. Wapenzi hao walikimbia, lakini walikamatwa baada ya miezi tisa kwenye mpaka wa Croatia na Montenegro na kurudishwa Uhispania.

Mahakama iliwataja wanandoa hao kuwa ni Tatania na Estanislao, lakini walitambuliwa na vyombo vya habari vya Uhispania kama Priscila Guevara na Constantín Dumitru.

Kulingana na mahakama, Tatania aliingia katika hoteli ya kifahari ya Atrio mnamo Oktoba 2021 kwa kutumia pasipoti bandia ya Uswizi. Baadaye alijiunga na Estanislao na wote wawili walifurahia mlo katika mgahawa huo wa Michelin star.

Lakini Estanislao alirudi asubuhi na mapema ili kuiba mvinyo kwa kutumia ufunguo ulioibwa, wakati ambao Tatania alikuwa mapokezi akizuga.

Aidha kulingana na gazeti la El País, wanandoa hao waliripotiwa kutembelea mgahawa huo  mara tatu kabla ya kufanya wizi huo. pia wameagizwa kulipa zaidi ya €750,000 kwa uharibifu.

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags