Wanafunzi 11 wauawa katika ajali ya moto, Uganda

Wanafunzi 11 wauawa katika ajali ya moto, Uganda

Takriban wanafunzi 11 wamekufa na wengine sita wako katika hali mbaya baada ya moto kuzuka katika shule ya walemavu wa macho katikati mwa Uganda.

Polisi ya Uganda imesema moto ulitokea saa saba usiku wa kuamkia jana katika shule ya Salaama, iliyoko Mukono, takriban kilomita 30 mashariki mwa mji mkuu Kampala. Polisi imeendelea kueleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Mara nyingi matukio ya moto hutokea katika shule za mabweni nchini Uganda, na aghalabu hulaumiwa kwa makosa ya uunganishaji wa nyaya za umeme. Lakini mamlaka inasema baadhi ya matukio hayo huanzishwa kwa makusudi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags