Usiku wa kuamkia leo Machi 3, 2025 limefanyika tukio la ugawaji wa tuzo kubwa duniani za Filamu za Oscar katika Ukumbi wa Dolby Theatre Ovation, Hollywood Los Angeles. Tuzo hizo zimefanyika ikiwa ni mara 97 tangu kuanziashwa kwake mwaka 1929.
Katika hafla hiyo, ambayo imehudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu duniani akiwemo Lupita Nyong'o anayewakilisha Kenya na Mexico. Baadhi ya waigizaji walifanikiwa kuibuka washindi wa tuzo kutoka kwenye vipengele tofauti tofauti ikiwa ni kati ya vipengele 24 vilivyokuwa vikiwaniwa usiku huo. Ifuatayo ni orodha ya washindi.
Filamu ya Anora iliyotoka mwaka 2024, yenye maudhui ya Mapenzi na Ucheshi iliyochezwa na Mikey Madison ndio iliibuka kinara baada ya kuchukua tuzo nyingi zaidi, ikifanikiwa kubeba tuzo tano ndani ya usiku mmoja. Filamu hiyo ilishinda tuzo ya Picha Bora, Mwigizaji Bora wa Kike akishinda 'Mikey Madison', Muongozaji Bora akishinda Sean Baker, Uhariri Bora, na Mwigizaji Bora Asilia.
Adrien Brody ameshinda tuzo ya Muigizaji Bora kupitia filamu ya 'The Brutalist' ambayo iliachiwa mwaka 2024, ikiwa na maudhui ya maigizo ya kihistoria ikielezea zaidi vita vya pili vya dunia. Kwa muigizaji Brody hii inakuwa Oscar yake ya pili ambapo mwaka 2003, akiwa na umri wa miaka 29 alifanikiwa kushinda Oscar kama muigizaji bora kupitia filamu ya The Pianist na kuweka rekodi ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kushinda kipengele hicho.
Hata hivyo, Filamu ya The Brutalist ilikuwa ikiwania vipengele kumi kwenye tuzo za Oscar 2025 lakini ilifanikiwa kushinda tuzo tatu ambazo ni Muigizaji bora wa kiume 'Adrian Brody' aliyeshinda kupitia filamu hiyo, Best Origin Score 'Alama bora asilia' aliyo shida muigizaji 'Daniel Blumberg' na Sinema bora zaidi 'Best Cinematography'.
Filamu ya 'Emilia Perez' iliyotoka mwaka 2024, ambayo ilikuwa akiwania vipengele 13 kwenye tuzo hizo za Oscar 2025, ilifanikiwa kuondoka na tuzo mbili usiku wa jana ambapo imeshinda kama filamu yenye wimbo bora wa asili na Kipengele cha mwigizaji Bora wa kike aliyesaidia tuzo ambayo ilienda kwa mwana dada Zoe Saldana kupitia filamu ya Emilia Perez. Katika tuzo za Oscar mwaka 2025, filamu ya Emilia Perez ndio ilikuwa ikiwania vipengele vingi zaidi.
Tuzo ya Muigizaji Bora wa kiume Anayesaidia 'Best Supporting Actor' imeenda kwa Kieran Culkin kupitia filamu ya A Real Pain ya mwaka 2024. Lakini pia kwa kipengele cha 'Best Costume Design' ameshinda Paul Tazewell ambaye kaweka rekodi ya kuwa Mwanaume wa kwanza Mweusi kushinda tuzo ya Ubunifu Bora wa Mavazi kwa watu wanaogiza kikatili kwenye filamu.
Tuzo ya Filamu Bora ya kimataifa imechukuliwa na 'Im Still Here' iliyotoka 2024, ikiigizwa na Fernanda Torres. Ushindi wa 'Im Still Here' umefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa filamu ya kwanza ya Kibrazil kushinda katika kipengele cha Best International Feature Film iliyokuwa ikiwania na filamu nyingine kubwa ambazo ni A Girl With The Needle, Flow, Emillia Peres, The Seed of the Sacred Fig.
Tukio lingine kubwa lakusisimu lililotokea usiku wa jana kwenye ugawaji wa tuzo za Oscar ni baada ya mtayarishaji nguli wa muziki nchini Marekani Quincy Jones kutunukiwa tuzo ya Muziki wa kusisimua kupitia filamu ya The Colour Purple iliyotoka 2025. Tuzo hiyo ilikuwa kwa ajili ya heshima kwa Jones aliyefariki Novemba, 2024, akiwa na umri wa miaka 91.

Leave a Reply