Waliofariki kwa kimbunga Freddy wafikia 400

Waliofariki kwa kimbunga Freddy wafikia 400

Idadi ya watu waliofariki kwa mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Freddy wapata 400, ambapo idadi hiyo inajumuisha vifo vilivyotokea tangu kimbunga hicho kilipoingia barani Afrika, Februari 2023, ambapo watu 326 ni kutoka Malawi , 53 kutoka Msumbiji na wengine 27 kutoka Madagascar.  

Wizara ya maliasili na mabadiliko ya hali ya hewa imesema licha ya dhoruba hiyo kutoweka, bado mvua kubwa zinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo, utabiri unaonesha huwenda zikasababisha mafuriko zaidi katika maeneo ya ziwa.

Rais kutoka nchini Malawi, Lazarus Chakwera alitembelea hospitali ya Queen Elizabeth na kukutana na wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwasaidia.

Aidha kwa takwimu za leo Machi 17, 2023, Kimbunga Freddy kimejeruhi zaidi ya watu 700 nchini Malawi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post