Wachezaji 62 wafungiwa kwa kudanganya umri

Wachezaji 62 wafungiwa kwa kudanganya umri

Shirikisho la ‘soka’ nchini Cameroon limewafungia wachezaji 62 kujihusisha na michezo baada ya kudanganya umri akiwemo mchezaji wa ‘klabu’ ya Victoria United, Wilfried Nathan Douala ambaye alikuwa katika kikosi cha Cameroon katika michuano ya Afcon 2023.

Douala alitanjwa kuwa mchezaji pekee mwenye umri mdogo ambapo alidai kuwa na umri wa miaka 17, Hata hivyo uchunguzi wa (FECAFOOT) umegundua umri halisi wa Douala ambao mpaka kufikia sasa haujawekwa wazi.

Aidha Douala anakabiliwa na uwezekano wa kupigwa marufuku kwa muda mrefu kushiriki ‘mechi’ katika ngazi ya kimataifa kwa udanganyifu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags