Vanessa Mdee aweka wazi juu ya utajiri wake

Vanessa Mdee aweka wazi juu ya utajiri wake

Na Habiba Mohamed

Hellow niaje niaje! Kama kawaida kila kona kutafuta  story moto moto na kukusogezea mdau wetu wa nguvu.Ebwana majina yanaumba  mnamkumbuka yule mwanadada wa Cash Madame ,Vee Mtonyo maarufu kama Vanesaa Mdee au Mama Seven.

Kama tunavyofahamu mwadada huyo aliachana na kabisa  na biashara ya muziki na kuelekeza nguvu zake katika ulezi wa mtoto aliyezaa na star maarufu  Rotimi kutoka Nigeria ambaye makazi yake yako nchini Marekani.

Mwadada huyo ameshare video kwenye ukurasa wake wa Instagram, katika video hiyo ikionyesha nyumba mpya nakuandika ujumbe ufuatao,

“This investment life is great GOD WE GIVE YOU THE GLORY Another one of our homes, built from ground up, furnished and ready to make money,forthebetter” Vanessa ameandika

kwa wenzangu na mie alimaanisha“Maisha haya ya uwekezaji ni mazuri Mungu tunakupa utukufu, Nyumba yetu nyingine, iliyojengwa kuanzia chini, iliyopambwa na tayari kutengeneza pesa ,usisahau kutizama video zetu forthebetter”

Alooooh!haya walimwengu  tumepata jibu la swali tulokuwa tukijiuliza baada ya mwadada huyu kuacha mzikii atafanya nini na jina la Cash Madame litakufa au vipi, Mama Seven kashatusanua kuhusu biashara yake na mafanikio yake.Shusha comment yako hapo chini utueleze unaweza jeh kufanya Maisha yako ya kila siku kuwa pesa kama staa huyo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post