Utumbo wa nguruwe wamponza kijana Paulo

Utumbo wa nguruwe wamponza kijana Paulo

Kijana mmoja alietambulika kwa jina la Paulo mapunda mkazi wa kijiji cha kipingu Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe anasurika kifo baada kukatwa mguu wake wa kulia na Mamba wakati akisafisha utumbo wa nguruwe kandokando ya Mto Ruhuhu.

Alisema mapunda siku ya Januari mosi  mwaka huu majira ya saa tano asubuhi nyumbani kwake kulikuwa na sherehe ya kipaimara hivyo walichinja nguruwe ambapo yeye alichukua utumbo kwenda kuusafisha Mtoni hapo huku akiwa ndani ya mtumbwi ndipo Mamba akajitokeza na kubinua mtumbwi kisha yeye kuangukia ndani ya maji.

Alieleza kuwa Mamba alikamata mguu wake wa kulia na kumzamisha kwenye maji lakini alijitahidi kuushikilia mtumbwi huku wakivutana na yeye akipiga kelele za kuomba msaada ndipo Watu walipojitokeza na kumsaidia kutowa ndani ya maji lakini mamba alishaukata mguu na kuondoka nao.

Hadi sasa amekwisha patiwa matibabu ya awali na anatakiwa kufanyiwa upasuaji lakini anashindwa kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha kupata matibabu hayo, ata hivyo ameiyomba serikali iwasaidie kupeleka mabomba ya maji ilikuepukana na majanga hayo ya kuliwa na mamba






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags