Utofauti kati ya Twitter na Threads

Utofauti kati ya Twitter na Threads

Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram Jana Alhamis Julai 6, 2023 imezindua mtandao wake mpya wa kijamii wa Threads unaofananishwa na Twitter katika matumizi na muundo wake.

Swali ambalo limeibuka miongoni mwa wadau na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni je, Threads itaweza kuiangusha Twitter? Mwananchi Scoop imekuandalia baadhi ya tofauti zilizopo kati ya mitandao hii miwili ya kijamii.

Threads inaruhusu mtumishi kuandika maneno 500 katika posti moja wakati Twitter kwa mtumiaji ambaye hajawa verifaidi' (hana tiki ya buluu) mwisho wa maneno ni 280 tu.

Pia, mtumishi wa Threads anaweza kuhamisha utambulisho wake (Biography) kutoka katika akaunti yake ya Instagram na kuitumia katika mtandao huo wakati Twitter haiwezekani.

Mtandao wa Twitter katika ukurasa wa nyumbani (Home page) mtumiaji anapata matukio na posti za watu wengine wakati katika Threads kwa sasa kuna ukomo katika Home page.

Hizo ni baadhi ya tofauti zilizopo kati ya Twitter na Threads, endelea kuwa karibu na mitandao yetu ya kijamii.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags