Utafiti, Paka wanamatendo yanayo fanana na Binadamu

Utafiti, Paka wanamatendo yanayo fanana na Binadamu

Utafiti kutoka katika Chuo Kikuu cha California Los, Angeles nchini Marekani (UCLA) umeeleza kuwa paka wana zaidi ya mionekano 200 ambayo wanyama hao hutumia kuwasiliana wao kwa wao.

Kwa mujibu wa BBC inaeleza kuwa watafiti hao waligundua kuwa paka wana matendo yanayo fanana na binadamu, na wanaweza kuwa wameichukua kutoka katika historia yao ya miaka 10,000 waliyoishi na binadamu.

Aidha watafiti hao 'walirekodi' mionekano ya uso wa paka kwa takribani dakika 194 na kugundua sura 276 tofauti tofauti za uso wao.

Ambapo kila muonekano wa paka ulitengenezwa kitofauti kama vile midomo wazi, mboni za macho kufumba na kufumbua, pua zinavyofunguka, masharubu na kusimama kwa masikio.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags