Na Michael ANDERSON
Tanzania kuna tatizo la baadhi ya vijana kuchagua kazi. Tatizo hili ni kubwa hasa kwa vijana wakiume. Baadhi yao wanaogopa kufanya kazi fulani kama mama lishe kwa kuogopa mitazamo ya jamii.
Uoga huu unaotokana na tabia na tamaduni zetu ambazo kijana wakiume akifanya kazi fulani hadhi na heshima yake inashuka katika jamii.
Hii imekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya vijana, kwani mitazamo ya jamii imewazuia kufanya kazi fulani ambazo zingeweza kuwapatia kipato. Mitazamo hii ya jamii imekuwa kizingiti kikubwa kwa baadhi ya vijana wasomi hasa wale waliopata nafasi ya kumaliza chuo kikuu.
Jamii imekuwa na tabia ya kuweka mategemeo makubwa kwa kijana kwamba akimaliza chuo ni lazima aajiriwe na afanye kazi katika ofisi yenye kiyoyozi na inayolingana na elimu yake.
Je, ni nini unachoweza kufanya kama mwanachuo ili kuongeza uwezekano wa kupata kazi?
Mchakato wa kutafuta kazi unapaswa uanze mapema, hata kabla ya kuhitimu.
Je wewe ni mwanachuo? Kama jibu ni Ndiyo, basi unaweza kuanza kutafuta fursa za kazi mapema mtandaoni au kwa kushiriki katika programu, miradi, semina, kuandaa projects na kujitolea katika makampuni.
Kwa kushiriki na watu wengine utapata kuongeza marafiki wapya (connection) ambao baadae wanaweza kuwa ndio daraja lako la kupata kazi.
Ni nini kinachotarajiwa kutoka kwako katika soko la ajira?
Unaweza kujenga mtandao wako wa kijamii (networking) kwa kuwa na mahusiano mazuri na walimu, wanafunzi wenzako na wataalamu wa tasnia yako.
Kupitia mtandao huu, utaweza kupata taarifa za kazi pale zinapopatikana. Hapa nina maanisha uwe na watu ambao watakuwa wana-support kile unachokifanya. Ukiishi na watu ambao hawa-support unachokifanya maana yake hakuna kazi utapata kupitia wao.
Nifanye nini ili nitambulike na niweze kupata kazi?
Kujitangaza ni muhimu sana katika ulimwengu wa kidigitali hasa unapokuwa kwenye harakati za kutafuta kazi.
Wewe mwanachuo unapaswa kuwa na ujuzi wa kujielezea mwenyewe katika majukwaa ya aina yoyote iwe kwa maandishi au kwa kuongea.
Kujifunza jinsi ya kuwa mbele kiujuzi na kimaarifa kunaweza kukusaidia kuwa na ujasiri, uwezo wa kuwasilisha mawazo, kushawishi waajiri wakupe kazi.
Asilimia 90 ya mazungumzo mtandaoni huwa ni kwenye maandishi hivyo ni bora kuwa vizuri zaidi kwenye uandishi.
TAKE NOTE!
Mtu yeyote mwenye kutafuta afueni ya maisha yake, yambidi afanye bidii na juhudi zote katika kutatua matatizo yanayoisibu tasnia yake.
Leave a Reply