Usalama wa hisia kwa mwanamke katika mahusiano

Usalama Wa Hisia Kwa Mwanamke Katika Mahusiano

Hivi ushawahi sikia mwanaume anasema huyu mwanamke nimempa kila kitu, pesa, nyumba, magari lakini bado simuelewi. (hajajua njia sahihi za kulinda hisia za mkewe)

Au ushawahi sikia mwanamke anasema huyu mwanaume hanijali, lakini ukiangalia unaona kabalikiwa kila kitu. (anatafuta ulinzi wa hisia)

Pia ushawahi sikia mwanamke anasema kama kuchepuka sawa ila niheshimu. (anatafuta ulinzi wa hisia zake)

Ushawahi simuliwa kwamba mwanaume anatoka nje ya ndoa lakini anamwambia mchepuko siku tukakapoachana ni pale mke wangu atakapojua nipo na wewe. (analinda hisia za mkewe)

Hisia za mwanamke zimejificha katika vitu vidogo sana.

Mwanamke anaweza kuumwa, mme akatoka akaenda kununua chakula cha gharama na kizuri akamletea mke ila mke asiwe na furaha. (hili jambo halijalinda hisia zake)

Na ukasikia analalamika kwako au kwa watu wengine kwamba hata niumwe vipi mme wangu hawezi hata nipikia hata uji na gesi ipo.(ulinzi wa hisia zake upo hapa)

Lakini ukumbuke huyu mwanaume kaonesha kujali kanunua mpaka chakula hotelini!

Ila ndiyo hajagusa hisia za mkewe.

Unaweza kumfanyia birthday party mkeo nzuri na asifurahie kwa sababu tu hujampost status

Wengi tunashindwa kumeet hisia za wake zetu kwa sababu tu hatujajua zipo wapi.

Na wanasaikolojia tunasema hisia za mpenzi wako nyingi zipo juu ya malalamiko yake juu yako.

Kile anachokulalamikia ndiyo ulinzi wa hisia zake ulipo.

Hata katika mapenzi wengi wanajua hisia za mwanamke zitakuja kwa kushikwa shikwa maeneo fulani. kama hujagusa maeneo ya ulinzi wa hisia zake basi jua anaweza kuwa numba na akaona kila kitu ni kero.

Sasa basi kati ya malengo yako 2021 katika ndoa yako au mahusiano yakow ewe kijana ni kujua ulizi wa hisia za mweza wako zipo wapi?

Orodhesha malalamiko yote juu yako kutoka kwake, anza kuyafanyia kazi.
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Janeth Jovin

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on business, money management on Tuesday and health on Thursday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include KARIA and FASHION.

Latest Post